Pablo: Kesho tunakwenda kubadili historia

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema kesho tunakwenda kubadili historia ya kufanikiwa kutinga Fainali ya Michuano ya Mapinduzi mara nyingi lakini tumeshindwa kuchukua taji.

Katika miaka saba iliyopita tumefanikiwa kutinga fainali mara tano lakini tumeshinda ubingwa mara moja pekee suala ambalo Pablo amesema kesho ni mwisho.

Pablo amefunguka kuwa kuingia fainali ni jambo zuri lakini kutwaa kombe ni vizuri zaidi hivyo tutahakikisha tunapambana hadi mwisho na kufanikiwa kushinda.

“Tangu mara ya kwanza nilivyokuja hapa nilisema malengo yetu ni kutwaa ubingwa, kesho ni fainali na tuko tayari kupambana kuhakikisha tunafikia dhamira hii.

“Wachezaji wote wako kwenye hali nzuri, tunategemea mchezo mzuri kama ulivyokuwa katika mechi dhidi ya Namungo. Tunataka kuibadili historia na kushinda taji,” amesema Pablo.

Kwa upande wake Nahodha Msaidizi Shomari Kapombe, amesema kila mchezaji yuko tayari kwa ajili ya fainali na lengo ni kutwaa taji.

“Tunajua kila tukifika fainali huwa tunapoteza. Katika miaka ya karibuni tumekuwa hatuna bahati na fainali lakini kesho tutabadili kila kitu,” amesema Kapombe.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER