Kikosi cha timu yetu Wanawake Simba Queens, leo kimeingia kambini kujiandaa na mchezo wa pili wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) dhidi ya Oysterbay Queens utakaopigwa Jumatatu Uwanja wa Mo Simba Arena.
Simba Queens itaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi mnono wa mabao 15-0 tuliyopata kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Ruvuma Queens.
Meneja wa Timu, Seleman Makanya amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri hakuna aliyepata maumivu katika mechi yetu ya kwanza.
Makanya amesema malengo yetu ni kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mechi zetu ili kutetea ubingwa.
“Kikosi kimeingia kambini leo kujiandaa na mchezo dhidi ya Oysterbay Queens utakaopigwa Jumatatu, wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri,” amesema Makanya.