Kocha Msaidizi, Seleman Matola, amesema mchezo wa hatua ya tatu ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) ulikuwa mgumu ila tunashukuru tumefanikiwa kushinda na kutinga 32 bora.
Matola amesema mechi za mtoano ni ngumu kwa sababu unapaswa kucheza kwa umakini muda wote kwani kosa moja tu linaweza kukufanya kutolewa mashindanoni.
Matola ameongeza kuwa ilibidi kufanya mabadiliko ya kikosi katika mchezo wa leo kutokana na kucheza mechi mfululizo hivyo ililazimika kupumzisha baadhi ya wachezaji.
“Tangu tulivyocheza na Red Arrows zimepita siku 10 na baada ya hapo tukacheza mechi kubwa dhidi ya Yanga kwa hiyo tulitumia nguvu nyingi.
“Tunacheza kila baada ya siku mbili na hivi tunavyozungumza Desemba 18 tunacheza mechi na Kagera Sugar mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, hivyo lazima tufanye mabadiliko ya mara kwa mara ya kikosi,” amesema Matola.
One Response