Timu yetu ya Simba Queens inaendelea na maandalizi kuelekea msimu mpya wa Ligi ya Wanawake ya (Serengeti Lite Women’s Premier League) ambao utaanza Desemba 23.
Zimebaki siku 10 kuelekea kufunguliwa kwa pazia la michuano hiyo Simba Queens chini ya kocha mzoefu Sebastian Nkoma iko kamili kuhakikisha tunafanya vizuri.
Lengo letu la kwanza msimu huu ni kutetea ubingwa wetu ambapo tumeshinda mara mbili mfululizo.
Ratiba ya mechi zetu tano za mwanzo
23/12/ 2021 Simba Queens vs Ruvuma
28/12/2021 Simba Queens vs Osterbay Girls
03/01/2022 Ilala Queens vs Simba Queens
08/01/2022 Yanga Princess vs Simba Queens
12/01/2022 Alliance Girls vs Simba Queens