Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema mchezo wa kesho wa Azam Sports Federation Cup dhidi ya JKT Tanzania ni muhimu kwetu kupata ushindi sababu tuna malengo makubwa na michuano hiyo.
Pablo amesema baada ya mchezo mgumu uliopita dhidi ya Yanga anatarajia kufanya mabadiliko kidogo kwenye kikosi kwa kupumzisha baadhi ya wachezaji ambao walicheza.
Pablo ameongeza kuwa tumetoka kucheza mechi ambayo tumetumia nguvu nyingi na iliyokuwa na presha kubwa pia tumepata muda mfupi wa kujiandaa kabla ya mchezo wa kesho kwa hiyo lazima tufanye mabadiliko ya kikosi kidogo.
“Jana tulifanya mazoezi ya kuweka sawa miili ya wachezaji (recovery) leo tutafanya mazoezi ya mbinu na kesho ndiyo mechi yenyewe kwa hiyo muda ni mfupi lakini ni mechi muhimu kwetu na tunahitaji kushinda.
“Kama nilivyowahi kusema Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wazuri hivyo nategemea kufanya mabadiliko ya kikosi, wale ambao hawakupata nafasi katika mchezo uliopita wanaweza kuanza na wengine wakasubiri kwenda kutoa msaada utapohitajika,” amesema Pablo.
One Response