Mechi dhidi ya watani wetu Yanga imemalizika kwa sare ya bila kufungana huku tukicheza soka safi na kutawala sehemu kubwa ya mchezo kitu ambacho kiliwachanganya wapinzani wetu.
Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zote zikionekana kucheza kwa tahadhari wakati mpira ukichezwa zaidi katikati ya kiwanja.
Washambuliaji wa timu zote mbili hawakupata huduma nzuri kutoka kwa viungo wao kipindi cha kwanza na kufanya walinda milango wawe likizo muda mrefu.
Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuwashambulia zaidi Yanga ambapo dakika 15 za mwanzo tulifanya mashambulizi matatu ya nguvu langoni mwao.
Dakika ya 87 nusura tupate bao na kuondoka na alama zote tatu kutoka kwa Sadio Kanoute aliyepiga shuti kali liliokolewa na mlinda mlango wa Yanga.
Kocha Pablo Franco aliwatoa Kibu Denis, Medie Kagere na Bernard Morrison kuwaingiza Rally Bwalya, Yusuph Mhilu na John Bocco.
2 Responses
Bahadhi ya wachezaji wametuangusha
Pia sub ya BM3, kocha alizingua
Bocco ameisha zeeka