Zikiwa zimebaki siku tano kabla ya mchezo wetu dhidi ya watani Yanga SC utakaopigwa Desemba 11 Uwanja wa Benjamin Mkapa tayari uongozi umeweka hadharani viingilio.
Viingilio vimepangwa Sh 5,000 kwa viti vya kijani,
Viti vya Bluu na machungwa Sh 7,000, VIP C Sh 15,000, VIP B Sh 20,000 na VIP A Sh 30,000.
Tiketi tayari zimeanza kuuzwa kupitia mitandao ya simu ili kuondoa usumbufu kwa mashabiki siku ya mechi.
Mashabiki kutoka mikoani watapata tiketi kupitia kwenye ofisi zote za TTCL zilizo karibu nao.
One Response