Tumetinga Makundi Shirikisho Afrika

Licha ya kupoteza kwa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Red Arrows tumefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na uwino wa mabao ya kufunga.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam tuliibuka na ushindi wa mabao 3-0 hivyo tumefuzu kwa jumla ya 4-2.

Katika mchezo wa leo, tulianza taratibu huku tukifanya mashambulizi machache ya kushtukiza na kuwaacha Arrows kumiliki sehemu kubwa.

Patrick Banda aliipatia Red Arrows bao la kwanza dakika ya 44 kwa shuti kali la mguu wa kushoto nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango Aishi Manula.

Arrows walirudi kwa kasi kipindi cha pili ambapo walifanikiwa kupata bao la pili dakika ya 47 lililofungwa kwa kichwa na Saddam Phiri.

Hassan Dilunga alitupatia bao la pekee dakika ya 67 baada ya kumzidi ujanja mlinzi wa Arrows kufuatia pasi iliyopigwa na Rally Bwalya.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Bernard Morrison, Bwalya, Medie Kagere na Dilunga kuwaingiza Shomari Kapombe, Joash Onyango, Mzamiru Yassin na John Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER