Mshambuliaji Medie Kagere na Bernard Morrison wamepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows utakaopigwa Uwanja wa Heroes hapa Zambia saa 10 jioni.
Wawili hao wamekuwa na uelewano mkubwa uwanjani kitu ambacho benchi letu la ufundi chini ya Kocha Pablo Franco limeamua kuwaanzisha pamoja.
Kagere na Morrison watapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Rally Bwalya pamoja na Hassan Dilunga.
Henock Inonga na Pascal Wawa watasimama kama mabeki wa kati wakipata ulinzi kutoka kwa viungo wakabaji Jonas Mkude na Sadio Kanoute.
Kikosi kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Pascal Wawa (6), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Hassan Dilunga (24), Sadio Kanoute (13), Medie Kagere (14), Rally Bwalya (8), Bernard Morrison (3).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Shomari Kapombe (12), Gadiel Michael (2), Joash Onyango (16), Erasto Nyoni (18), Peter Banda (11), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22) Ibrahim Ajibu (10).
One Response