Tuko tayari kupeperusha bendera ya nchi kimataifa

Kikosi chetu kiko tayari kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows utakaopigwa katika Uwanja wa Heroes hapa jijini Lusaka, Zambia saa 10 jioni kwa saa za nyumbani.

Wachezaji wote 25 waliosafiri waki ya kamili na jana wamefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa mchezo wa leo.

Majibu ya vipimo vya Covid-19 yalitolewa jana baada ya kikao cha maandalizi ya mchezo (Pree match meeting) na msafara wetu wote wakiwamo wachezaji wote 25 hakuna aliyekutwa na maambukizi.

KOCHA PABLO

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesisitiza kuwa katika mchezo wa leo tunapaswa kuwa makini kutumia nafasi tutakazopata, kuimarisha ulinzi na kupunguza makosa ili tupate ushindi.

Pablo amesema anapenda kufuzu hatua za makundi kwa ushindi hivyo amewataka wachezaji kuhakikisha wanatumia vyema kila nafasi itakayopatikana na walinzi nao kuwa makini kuwazuia Red Arrows.

“Nategemea mchezo utakuwa mgumu, tunajua wataingia kwa kushambulia kuanzia mwanzo lakini nisingependa kufuzu hatua inayofuata kwa kupoteza au kuteseka.

“Simba ni timu kubwa, ina wachezaji bora, tunaenda kucheza kwenye uwanja mzuri kwa hiyo kama Simba lazima tufikirie ushindi,” amesema Pablo.

BARBARA ASEMA HAKUNA ZAIDI YA KUINGIA MAKUNDI

Mtendaji Mkuu wa klabu Barbara Gonzalez amesema katika mchezo wa leo hakuna kingine chochote tunachohitaji zaidi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hii.

Barbara amesema tunafahamu mchezo utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kufuzu hatua inayofuata hasa tukiwa na mtaji mzuri wa mabao 3-0 tuliopata nyumbani.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER