Simba kuifuata Ruvu Shooting leo

Kikosi chetu kitaondoka leo jioni kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Novemba 19 Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.

Baada ya mapumziko ya wiki mbili kupisha mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Dunia ligi inarejea na mchezo wetu wa kwanza utakuwa Ijumaa dhidi ya Ruvu Shooting.

Katika kipindi chote cha mapumziko timu ilikuwa inaendelea kunafanya mazoezi na iliingia kambini Jumatatu kujiandaa na mchezo huo ambao tunatarajia utakuwa mgumu.

Mchezo wa Ijumaa utakuwa ni wa kwanza kwa Kocha Mkuu Pablo Franco raia wa Hispania tangu alipoanza kazi ya kukinoa kikosi chetu mapema mwezi huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER