Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema moja ya sababu iliyoifanya Timu yetu ya Taifa ya Tanzania kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa DR Congo jana ni kushindwa kutumia nafasi tulizotengeneza.
Pablo ambaye alikuwepo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mchezo huo, amesema kitendo cha kupoteza idadi ile ya mabao kiliwapa nguvu wageni na kuwafanya wenyeji kucheza kwa presha.
Raia huyo wa Hispania ameongeza kuwa Taifa Stars inacheza vizuri na ina muunganiko mzuri kuanzia nyuma hadi mbele ila changamoto imebaki kwenye umaliziaji.
“Si matokeo mazuri kwa Watanzania na yanaumiza lakini walicheza vizuri, walimiliki mpira muda mrefu shida ikawa ni kumalizia, hilo nalo limechangia kupoteza mechi. Wapinzani waliruhusu Tanzania icheze na wao wakatumia nafasi walizopata,” amesema Pablo.
Aidha, Pablo amewasifu mlinda mlango Aishi Manula na walinzi Shomari Kapombe na Mohamed Hussein kwa kuonyesha kiwango safi katika mchezo huo.
“Aishi aliokoa mabao akiwa anatazamana na mpigaji, pia alipangua michomo kadhaa ni kipa mzuri, Shomari na Mohamed nimeona ni wazuri kwenye kukaba na kushambulia pia nimefurahi kuwaona,” amesema Kocha Pablo.
One Response