Dilunga Mchezaji Bora Simba Oktoba

Kiungo mshambuliaji, Hassan Dilunga, amechaguliwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa mashabiki wa Emirate Aluminium ACP kutokana na umahiri mkubwa aliouonyesha.

Katika mwezi Oktoba Dilunga ameshiriki mechi zote nne akiwa ameanza kikosi cha kwanza akicheza jumla ya dakika 320.

Dilunga amewapiku viungo wenzake Sadio Kanoute na Rally Bwalya ambaye alikuwa akimfukuzia kwa karibu.

Dilunga atakabidhiwa kitita cha fedha taslimu Sh. 2,000,000 kutoka kwa Emirate Aluminium ACP ambao ni wadhambini wa tuzo hiyo tangu walipoanza Februari mwaka huu.

Dilunga ameibuka mshindi baada ya kupigiwa kura nyingi zaidi ya wenzake na mashabiki kupitia Tovuti yetu rasmi ya klabu ya www.simba.co.tz.

Mchanganuo wa kura ulivyokuwa.

Dilunga kura 2249
Bwalya kura 2199
Kanoute kura 376

Dilunga 46.62%
Bwalya 45.58%
Kanoute 7.79%

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER