Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limeruhusu idadi ya mashabiki 15,000 kuhudhuria mchezo wetu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa utakaopigwa Oktoba 24 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
CAF imeweka utaratibu wa kuruhusu idadi ndogo au kuzuia kabisa mashabiki kuingia uwanjani kutokana na kudhibiti kusambaa homa ya virusi vya Corona.
Mara zote CAF imekuwa ikisisitiza taratibu zote za kujikinga na ugonjwa wa corona kufuatwa viwanjani.