Kagere arejesha tabasamu kwa mashabiki akiitungua Dodoma

Bao pekee lililofungwa na mshambuliaji Medie Kagere limetosha kutupa alama tatu muhimu dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa Uwanja Jamhuri.

Kagere alitupatia bao hilo dakika ya 68 akipokea pasi ya kichwa iliyopigwa na Chris Mugalu kufuatia mpira mrefu uliopigwa na mlinda mlango Aishi Manula.

Kiungo mshambuliaji Pape Sakho alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 11 baada ya kupata maumivu mguuni kwa kuumizwa na mlinzi wa Dodoma.

Dakika ya 43 mshambuliaji wa Dodoma, Anuary Jabir alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kiwiko Kennedy Juma ambaye naye alishindwa kuendelea na mchezo.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Dodoma lakini tulipoteza nafasi kadhaa.

Kocha Didier Gomes aliwatoa Sakho, Kennedy na Taddeo Lwanga nafasi zao zikachukuliwa na Rally Bwalya, Henock Inonga, John Bocco na Medie Kagere.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER