Simba kupaa mchana kuifuata Dodoma Jiji

Kikosi chetu leo mchana kinaondoka jijini Mwanza kwa Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kuelekea Dodoma kikipitia Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa pili wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji Ijumaa.

Kikosi kitafika Dar es Salaam jioni na kubadili ndege kabla ya kuanza safari ya kuelekea Dodoma tayari kwa mtanange huo.

Licha ya kuanza kwa sare katika mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Biashara United jana ieleweke kuwa wachezaji hawajachanganyikiwa na matokeo yaliyotokea.

Mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji utapigwa Uwanja wa Jamhuri, Ijumaa Oktoba Mosi saa 10 jioni mtanange ambao tunaamini utakuwa mgumu.

Mchezo dhidi ya Dodoma ni muhimu kwetu na tunahitaji kupata alama tatu ili kurejesha imani ya mashabiki hasa baada ya mechi mbili zilizopita kutofanya vizuri.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER