Mugalu kuongoza mashambulizi dhidi ya Yanga, Sakho Kanoute ndani

Mshambuliaji Chris Mugalu amepangwa kuongoza mashambulizi dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga leo ambao utaanza saa 11 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mara nyingi kocha Didier Gomes amekuwa akipenda kumtumia Mugalu kuongoza mashambulizi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukaa na mpira mguuni.

Mugalu atasaidiwa kwa ukaribu na kiungo fundi Rally Bwalya ambaye atacheza namba 10 wakati Hassan Dilunga akitokea upande wa kushoto.

Kiungo Sadio Kanoute ambaye alionyesha kiwango safi katika mchezo dhidi ya TP Mazembe naye ataanza huku Pape Sakho akipewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Kikosi Kamili kilivyopangwa,

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6), Taddeo Lwanga (4), Pape
Sakho (17), Sadio Kanoute (13), Chris Mugalu (7), Rally Bwalya (8), na Hassan Dilunga (24).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma, Erasto Nyoni (18), Mzamiru Yassin (19), Peter Banda (11), John Bocco (22), Yusuph Mhilu (27).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER