Ni Simba VS TP Mazembe Simba Day

Katika kuadhimisha kilele cha Tamasha kubwa la Simba Day, timu yetu itacheza na mabingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amethibitisha usiku huu kwamba TP Mazembe ndiyo watakuwa wageni wa Simba safari hii.

“Nina furaha kuwatangazia Wanasimba na Watanzania wote kwa ujumla kwamba tutacheza na TP Mazembe siku ya Simba Day Septemba 19 mwaka huu.

” Tayari tumekamilisha taratibu zote za kuwaalika na sasa ni rasmi kwamba wao ndiyo watakuwa wageni wetu,” amesema Barbara.

Amesema TP MAzembe ni mojawapo ya timu zenye heshima kubwa barani Afrika na ni heshima kubwa kwa Simba kupata fursa ya kucheza nayo hapa nchini.

Barbara amesema lilikuwa lengo la uongozi na benchi la ufundi kuhakikisha Simba inapata timu nzuri ili kujua ni wapi hasa kikosi cha msimu huu kipo kwenye maandalizi ya msimu ujao wa ligi.

Barani Afrika, Mazembe inachukuliwa kama mojawapo ya vilabu bora na jina lake linahusishwa na mafanikio katika mchezo huo.

Taarifa zaidi kuhusu ujio wa Mazembe zitaendelea kutolewa na klabu kuelekea katika Wiki ya Simba na hatimaye Simba Day.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER