Mshambuliaji nyota wa timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens, Oppah Clement ataongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa Nusu Fainali ya Caf Women’s Champions League Cecafa Qualifiers 2021 dhidi ya Vihiga Queens utakaopigwa Uwanja wa Nyayo saa saba mchana.
Katika mchezo uliopita ambao ulikuwa wa mwisho hatua ya makundi Oppah na Mawete Musolo walifunga mabao matatu ‘hat trick’kila mmoja.
Oppah ni mshambuliaji kinara wa Simba Queens ambapo katika ligi ya Wanawake msimu uliopita amemaliza nafasi ya pili akifunga mabao zaidi ya 30.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
- Zubeda Mgunda
- Fatuma Issa
- Dotto Evarist
- Juliet Singano
- Violeth Nicholaus
- Danai Bhobho
- Mawete Musollo
- Joelle Bukuru
- Oppa Clement
- Asha Djafar
- Ruth Kipoyi
Wachezaji wa Akiba
- Gelwa Yona (Kipa)
- Janeth Shija
- Shelda Boniface
- Aisha Juma
- Maimuna Thomas
- Silivia Thomas
- Koku Kipanga
- Zena Khamis
- Violeth Thadeo
- Wema Richard