Barbara ashukuru mwitikio Simba App

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, amewashukuru wana Simba kwa namna walivyojitokeza kwa wingi kupakua Simba App.

Gonzalez alisema kitendo cha kupata watumiaji wa Simba App zaidi ya elfu 50 katika kipindi kifupi kimempa matumaini makubwa ya kupata watumiaji wengi zaidi huko mbele.

” Pamoja na changamoto kadhaa zilizojitokeza, bado wana Simba kwa wingi wao walijiunga na Simba App. Nawashukuru sana na ahadi yangu kwao ni kwamba tutaifanya Simba App iwe bora si Tanzania pekee bali Afrika kwa ujumla,” alisema.

Katika kipindi cha saa 72 zilizopita, Simba App ndiyo imekuwa application inayopakuliwa zaidi nchini Tanzania – ikizizidi hadi applications maarufu kama Livescore ambazo kwa utamaduni zimekuwa zikipakuliwa zaidi mwanzoni mwa misimu ya mashindano.

Barbara alitumia nafasi hiyo kuahidi kwamba changamoto kwa ajili ya watumiaji wa mitandao mingine ya simu tofauti na Tigo, Airtel na Vodacom kwenye kufanya malipo ya kujiunga zinashughulikiwa

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER