Kauli ya Kocha Hababuu kuelekea mchezo wa Kesho, Oppah arejea kundini

Kocha Mkuu wa Timu ya Wanawake ya Simba Queens, Hababuu Ally ameweka wazi kuwa tumejipanga kuhakikisha tunaibuka na ushindi dhidi ya Lady Doves kesho ili kujihakikishia kutinga nusu fainali ya michuano ya Caf Women’s Champions League Cecafa Qualifier 2021 inayoendelea hapa nchini Kenya.

Kocha Hababuu amesema Doves ni mabingwa wa Uganda na wana kikosi imara lakini tumejipanga kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kutinga nusu fainali.

Hababuu amesema maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri na wachezaji wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu kuelekea mchezo wa kesho.

“Tunahitaji kushinda kesho dhidi ya Lady Doves, tukishinda tutakuwa tumekata tiketi ya kuingia nusu fainali na malengo yetu ni kushinda taji hili baadaye twende Misri” amesema Kocha Hababuu.

Kocha Hababuu amethibitisha mshambuliaji nyota Oppah Clement amejiunga pamoja na wenzake na atakuwepo kwenye mchezo wa kesho baada ya kumaliza matatizo yake ya kifamilia.

“Oppah amejiunga na wenzake na atakuwepo kesho, ni mchezaji muhimu na tunaamini uwepo wake utaongeza nguvu kikosini.

“Pia tutakosa huduma ya wachezaji wetu wawili Wema Richard na Kadosho Shaban ambao ni majeruhi,” amesema Kocha Hababuu

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER