Mlinzi wa kulia Israel Patrick Mwenda, amejiunga na kikosi chetu akitokea Timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC).
Mwenda amekuwa kwenye kiwango bora msimu uliopita akiwa KMC hali iliyosababisha kulivutia benchi la ufundi chini ya Kocha Didier Gomes.
Licha ya uwezo mkubwa alioonyesha msimu huu pia umri wa Mwenda ni mdogo ambao unamruhusu kucheza soka kwa muda mrefu.
Mwenda anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa ndani ya kikosi chetu baada ya Peter Banda aliyetoka Big Bullet ya Malawi, Yusuph Mhilu kutoka Kagera Sugar, Duncan Nyoni, Ousmane Sakho na Henock kutoka DC Motema Pembe.
Bado tunaendelea kufanya usajili kwa umakini mkubwa kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi 2021/22.
2 Responses
jaribuni basi kuandika mchezaji amesain miaka mingapi wengne mnaweka wengine hamuweki dah
I appreciate the effort of our beloved coach Gomez Da Rosa