Benchi letu la ufundi na wachezaji wote wamepata chanjo ya ugonjwa wa corona kabla ya kuanza rasmi maandalizi ya msimu mpya wa ligi 2021/22.
Chanjo hiyo imetolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam leo mchana.
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais, Samia Suluhu Hassan inaendelea kuhamasisha watu kupata chanjo ili kujikinga na janga hilo ambalo linatikisa dunia kwa sasa.
Tayari wachezaji wameripoti kambini leo kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mshike mshike wa msimu mpya wa ligi.