Simba kuanza maandalizi ya msimu mpya Agosti 8

Kikosi cha Mabingwa wa Ligi Kuu na Michuano ya Azam Sports Federation Cup, kinatarajia kurejea mazoezini Agosti 8  kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi 2021/22.

Baada ya kikosi kurejea kutoka mkoani Kigoma kilipocheza fainali na kutwaa ubingwa wa FA kambi imevunjwa na wachezaji wamepewa mapumziko ya siku 10.

Kocha Mkuu Didier Gomes naye ameondoka kwenda nchini kwao Ufaransa kwa mapumziko kabla ya kurejea kuanza maandalizi ya msimu mpya.

Wachezaji wanaotoka nje ya nchi nao wamepewa ruhusa ya kwenda kwao kuziona familia zao kutokana na muda mfupi kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Timu inatarajia kwenda kuweka kambi nje ya nchi ingawa bado haijafahamika itakuwa wapi kwa sababu mchakato bado unaendelea.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER