Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam FC utakaopigwa kesho saa moja usiku katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Maandalizi ya mchezo yamekamilika na tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Azam lakini tumejipanga kuwakabili.
Ingawa tayari tumetawazwa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara lakini hatuwezi kubweteka tunahitaji kupata ushindi katika kila mchezo.
Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu na kila mmoja atakayepewa nafasi yupo tayari kuipigania timu.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa tulitoka sare ya kufungana mabao 2-2.