Baada ya mapumziko ya siku moja kikosi chetu leo jioni kimefanya mazoezi kwenye Viwanja vya Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo ujao wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union utakaofanyika Jumapili, Julai 11 saa moja usiku.
Baada ya ushindi wa mabao 2-0 tuliopata juzi Jumatano dhidi ya KMC wachezaji walipewa mapumziko kabla ya kuanza mazoezi leo.
Wachezaji wote wamehudhuria mazoezi na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao tunaweza kutangazwa rasmi mabingwa.
Katika mchezo huo tunahitaji kupata alama moja ili tutangazwe kuwa mabingwa kwa sababu tutafikisha pointi 77 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.