Ushindi wa mabao 2-0 tuliopata dhidi ya KMC leo, umetufanya tuzidi kuukaribia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Msimu wa 2020/21 kwa asilimia 99.
Kwa asilimia hizo tumeendelea kutetea ubingwa wetu ambapo hii inamaanisha kuwa hata kama tutapoteza mechi zetu tatu zilizosalia anayetufuatia atafikisha alama 76 sawa nasi lakini bado tutamzidi kwenye uwiano wa mabao.
Katika mchezo wa leo, Chris Mugalu alitupatia bao la kwanza mapema dakika ya pili baada ya kupokea pasi kutoka kwa Clatous Chama.
Mugalu alitupatia bao la pili dakika ya 45 baada ya kumalizia pasi iliyopigwa na Rally Bwalya na kupiga shuti la chini chini lililomshinda mlinda mlango Juma Kaseja.
Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuendelea kulisakama lango la KMC huku tukitawala mchezo na kutengeneza nafasi ingawa hatuweza kuzitumia.
KMC walimaliza dakika 10 za mwisho wakiwa pungufu baada ya mlinzi wake wa kati Andrew Vincent ‘Dante’ kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje.
Kocha Didier Gomes aliwatoa Mzamiru Yassin, Luis Miquissone na Mugalu na kuwaingiza Hassan Dilunga, Bernard Morrison na John Bocco.
Katika mchezo ujao dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Jumapili tunahitaji alama moja ambayo itatufanya kufikisha pointi 77 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote hatua itakayotufanya kuwa mabingwa.