Tunataka ubingwa wetu tu kwa KMC leo

Kikosi chetu leo kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC kwa lengo moja tu la kutetea ubingwa wetu kwa mara ya nne mfululizo.

Alama tatu kwenye mchezo wa leo zitatufanya kufikisha pointi 76 ambazo zinaweza kufikiwa na anayetufuata lakini uwiano wa mabao ya kufunga tumewaacha mbali hivyo kimahesabu tukishinda tunakuwa mabingwa.

Tukiibuka na ushindi leo dhidi ya KMC tutakuwa mabingwa huku tukiwa tumebakiwa na michezo mitatu mkononi.

Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na wachezaji wote wako vizuri.

“Mchezo utakuwa mgumu kwa sababu KMC wanahitaji alama tatu ili kujiweka nafasi nzuri kwenye msimamo kutokana ligi inaelekea ukingoni lakini tumejipanga kuwakabili. Sisi tunataka ubingwa na tukishinda tutakuwa mabingwa sababu wanaotufuata wakishinda mechi zao tutakuwa sawa lakini tumewazidi idadi ya mabao,” amesema Matola.

TAARIFA YA KIKOSI

Wachezaji wote wako kambini na wamefanya mazoezi hivyo inaipa nafasi nzuri benchi la ufundi kupanga kikosi kulingana na mahitaji ya mchezo.

MCHEZO ULIOPITA

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Desemba 16, mwaka jana tuliibuka na ushindi wa bao moja lililofungwa na Medie Kagere kwa mkwaju wa penati dakika ya 76.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER