Wametuchelewesha tu, ubingwa uko pale pale

Pamoja na kupoteza mchezo kwa bao moja mbele ya watani wetu Yanga lakini ni kama wametuchelewesha ila ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu huu ni suala la muda tu.

Kama tungepata alama tatu kwenye mchezo wa leo tungetangazwa mabingwa lakini kwa sababu imeshindikana basi tutajitahidi katika mechi zetu nne zilizobaki.

Yanga ilipata bao dakika ya 11 kupitia kwa Zawadi Mauya baada ya kupiga shuti kali lililomgonga mchezaji wetu na kumpoteza mlinda mlango, Aishi Manula.

Katika kipindi cha kwanza hatukutengeneza nafasi nyingi za kufunga kama kawaida kutokana na wapinzani kuwa wengi nyuma na kuziba njia.

Kipindi cha pili tulianza kwa Kasi na kumiliki mchezo muda mrefu huku tukitengeza nafasi ingawa changamoto ikawa kwenye kuzitumia.

Kocha Didier Gomes aliwatoa Erasto Nyoni, Clatous Chama na Taddeo Lwanga na kuwaingiza Rally Bwalya, Medie Kagere na Chris Mugalu.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. …WALAI WANA BAHATI SANAA WACHEZAJI WA SIMBA WALIKUWA COMMITED SANa …tunawaombea watupe raha Zaid ..#marefaree Ni kama nyama ya tembo Ni ngumu kuwaelewa kwa maamuz yao
    🎇🎆🏆🏆🏆🏆🏆🏆🏆🏆🏆

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER