Mlinda mlango namba moja, Aishi Manula na kiungo Taddeo Lwanga wamerejea kikosini na wanaanza kwenye mchezo wetu wa leo wa Nusu Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Azam FC baada ya kumaliza adhabu ya kadi tatu za njano.
Wawili hao waliukosa mchezo wa ligi uliopita dhidi ya Mbeya City kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano lakini leo wamerejea na Kocha Didier Gomes amewaanzisha wote.
Nahodha John Bocco ataendelea kuongoza idara ya ushambuliaji akisaidiwa kwa karibu na Clatous Chama, Luis Miquissone na Rally Bwalya.
Katika kiungo wa ulinzi Kocha Gomes amewapanga Taddeo na Mzamiru Yassin kutokana na ugumu wa mchezo wenyewe.
Kikosi kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6), Taddeo Lwanga (4), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Rally Bwalya (8) Luis Miquissone (11).
Wachezaji wa Akiba : Beno Kakolanya (30), David Kameta (27), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Hassan Dilunga (24), Medie Kagere (14), Bernard Morrison (3).