Kocha Mkuu Didier Gomes leo amewapanga washambuliaji wawili Nahodha John Bocco na Chris Mugalu kuanza katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Gomes amekuwa akitumia washambuliaji wawili katika mechi chache hasa za mikoani kutokana na aina ya wapinzani na uwanja unaotumika lakini amekuwa akiamini kwenye matumizi ya mshambuliaji mmoja.
Mlinzi Joash Onyango amerejea kikosini baada ya kupona majeraha aambapo atashirikiana na pacha wake Pascal Wawa.
Katika eneo la kiungo wa ulinzi Taddeo Lwanga atacheza na Mzamiru Yassin wakati Rally Bwalya na Luis Miquissone wakiwasaidia Bocco na Mugalu.
Kikosi Kamili kilivyopangwa dhidi ya Polisi Tanzania
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (15), Pascal Wawa (6), Taddeo Lwanga (4), Rally Bwalya (8), Mzamiru Yassin (19),John Bocco (c) (22), Chris Mugalu (7),
Luis Miquissone (11).
Wachezaji wa Akiba: Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Kennedy Juma (26), Hassan Dilunga (24), Bernard Morrison (3),Medie Kagere (14), Perfect Chikwende (23).