Kikosi chetu leo kimefanya mazoezi ya mwisho katika viwanja vyetu vya Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Juni 19, mwaka huu.
Baadhi ya wachezaji waliokuwa kwenye Timu ya Taifa wamefanya mazoezi pamoja na wenzao tayari kwa maandalizi ya mchezo huo.
Nyota Clatous Chama na Taddeo Lwanga wao bado hawajawasili nchini na wanatarajia kufika muda wowote kuanzia sasa huku Jonas Mkude suala lake likiwa halijamalizika.
Kikosi kitaondoka kesho mchana kwa ndege kuelekea jijini Mwanza tayari kwa mchezo huo.