Kikosi chetu cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, leo usiku kitashuka dimbani kuikabili JKT Tanzania katika mchezo ambao tunapaswa kushinda ili kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.
Alama tatu kwenye mchezo wa leo zitatufanya kufikisha saba ambazo zitatufanya kuingia nusu fainali bila kuangalia matokeo ya timu nyingine.
Kocha Mkuu, Nico Kiondo amesema amewaandaa vijana kimwili na kiakili kuelekea mchezo wa leo huku akiamini tunaweza kushinda ingawa haitakuwa mechi rahisi.
“Mechi ya leo itakuwa ngumu sababu inatoa maamuzi kuelekea nusu fainali lakini nimewaandaa wachezaji vizuri na ninaamini tutapata ushindi na malengo yetu ni kutwaa ubingwa,” amesema Kocha Nico.