Tumeanza kwa ushindi Ligi Kuu ya NBC

Mchezo wetu wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 dhidi ya Fountain Gate FC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa kuibuka na ushindi mabao 3-0.

Mlinzi wa kati, Rushine De Reuck alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya tano baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Jean Charles Ahoua.

Ahoua alitupatia bao la pili dakika ya 36 akiwa ndani ya sita baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na kiungo mkabaji, Yusuph Kagoma.

Jonathan Sowah alitupatia bao la tatu dakika ya 57 kwa shuti kali la mguu wa kushoto akiwa ndani ya sita baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Elie Mpanzu.

Mchezo wa Ligi unaofuata tutacheza dhidi ya Namungo Oktoba Mosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

X1: Camara, Kapombe (Duchu 72′), Naby, Chamou, De Reuck (Nangu 72′), Kagoma (Maema 64′), Kibu (Mourice 45′), Mzamiru (Kante 45′), Sowah, Ahoua, Mpanzu

Waliionyeshwa kadi:

X1: Kisunga, Jolam, Mokono, Kulandana, Lamela, Sadick, Kataga, Pandu, Mudrick, Shomari, Hassan (Ntambi 60′)

Waliionyeshwa kadi: Kulandana 90+2′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER