Tupo tayari kuanza msimu mpya wa NBCPL

Leo saa moja usiku kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Fountain Gate FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Huu ni mchezo wa kwanza wa Ligi kwenye msimu wa 2025/2026 ambao tumejipanga kuhakikisha tunapata alama zote tatu tukiwa katika Uwanja wa nyumbani.

Tutaingia kwenye mchezo wa leo kwa kuwaheshimu Fountain Gate ili kuweza kufikia malengo ya kupata alama tatu.

Matola afunguka kuhusu mchezo….

Kocha msaidizi, Seleman Matola amesema Ligi ya msimu huu itakuwa ngumu kutokana na kila timu kujipanga vizuri na tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Fountain Gate lakini tupo tayari kupambana kwa ajili ya alama tatu.

Matola ameongeza kuwa malengo yetu msimu huu ni kuhakikisha tunatwaa ubingwa wa Ligi kwahiyo tunapaswa kuanza vizuri kwa kupata alama tatu mbele ya Fountain Gate ingawa haitakuwa kazi rahisi.

“Maandalizi yetu yamekwenda vizuri na tupo tayari kuhakikisha tunapata alama tatu katika mchezo wa kesho dhidi ya Fountain Gate,” amesema Seleman.

Duchu aongea kwa niaba ya wachezaji….

Mlinzi wa kulia, David Kameta ‘Duchu’ amesema wapo tayari kufuata malekezo watakayopewa na walimu ili kuweza kufikia malengo ya kupata alama zote tatu nyumbani.

“Kila mchezaji anatambua kuwa hautakuwa mchezo rahisi lakini tupo tayari kuhakikisha tunafuata maelekezo tutakayopewa na walimu ili kuweza kupata alama tatu,” amesema Duchu.

Hali ya kikosi……..

Wachezaji wapo kwenye hali nzuri na tayari kwa mchezo wa leo isipokuwa tutaendelea kukosa huduma ya kiungo mshambuliaji, Mohamed Bajaber ambaye anaendelea kupata matibabu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER