Kikosi chetu kimefanikiwa kupata ushindi wa bao moja katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United uliopigwa Uwanja wa Obedi Itani Chilume nchini Botswana.
Elie Mpanzu alitupatia bao hilo pekee dakika ya 15 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na nahodha, Shomari Kapombe.
Baada ya bao hilo tuliendelea kutengeneza nafasi na kufanya mashambulizi huku wenyeji Gaborone wakifanya mashambulizi machache ya kushtukiza.
Kipindi cha wenyeji Gaborone walirejea kwa kasi kutaka kurejesha bao hilo lakini safu yetu ya ulinzi ilikuwa imara kuhakikisha tunakuwa salama.
Mchezo wa mkondo wa pili utapigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 28 na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya kwanza ya michuano hiyo.
X1: Motswagole, Velaphi, Ivan, Gora, Johnson, Ditsele, Phiri, Kgwasane, Maponda (Sesay 68′), Ramoagi (Chideu 80′) Kgamanyane (Pantev 89′)
Waliionyeshwa kadi: Gora 21′ Velaphi 31′
X1: Camara, Kapombe, Mligo, Chamou, De Reuck, Kante (Mzamiru 66′), Mpanzu (Mutale 90+2′) Naby (Nangu 88′) Mwalimu (Mukwala 66′) Ahoua, Maema (Kibu 66′)
Waliionyeshwa kadi: Naby 60′ Kapombe 82′