Nahodha wa timu, Shomari Kapombe amesema wachezaji wapo tayari kupambana hadi mwisho kuhakikisha tunapata ushindi dhidi ya Gaborone United kwenye mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kapombe amesema kila mchezaji yupo timamu asilimia 100 kuhakikisha anasaidia timu kupata ushindi muhimu ugenini.
Kapombe ameongeza kuwa itakuwa mechi ngumu kwa jinsi walivyowatazama wapinzani lakini aina ya kikosi tulichonacho na uzoefu wa michuano hii tuna nafasi kubwa ya kupata ushindi.
“Haitakuwa mechi rahisi lakini kwa upande wetu kama wachezaji tupo tayari kujitoa, kila atayepata nafasi ya kucheza atahakikisha anaisaidia timu kupata,” amesema Kapombe.