Fadlu: Tupo tayari kuanza safari ya Ligi ya Mabingwa

Kocha Mkuu, Fadlu Davids ameweka wazi kuwa kikosi chetu kipo tayari kuanza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2025/2026 hasa baada ya kupata maandalizi mazuri.

Fadlu ameyasema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na vyombo vya habari kuelekea mchezo wetu wa kesho wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United utakaopigwa Uwanja Obedi Itani Chilume nchini Botswana saa mbili usiku.

Fadlu ameongeza kuwa tumecheza mechi mbili zenye uzito mkubwa Simba Day dhidi ya Gor Mahia kutoka Kenya na Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga kwahiyo wachezaji wapo tayari kwa ajili ya ushindani.

Aidha Fadlu ameongeza kuwa anaiheshimu Gaborone United kwakuwa ni Mabingwa wa nchi yao lakini tumejipanga kwa ajili ya kushinda mechi zote nyumbani na ugenini ili tuweze kufuzu hatua inayofuata.

“Kwenda hatua ya makundi unahitaji kushinda mechi zote nyumbani na ugenini na sisi tumejiandaa kufanya hivyo. Timu yangu imecheza mechi mbili zenye uzito mkubwa Simba Day na Ngao ya Jamii kwahiyo wachezaji wangu wapo tayari kwa ushindani.”

“Hata hivyo namheshimu sana kocha wa upinzani pamoja na timu yake kwa ujumla kwa sababu nao Mabingwa kwahiyo tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tupo tayari kwa ushindani,” amesema Fadlu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER