Leo asubuhi kikosi chetu kimeondoka kuelekea nchini Botswana kwa ajili ya mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United utakaopigwa Jumamosi, Septemba 20.
Kikosi kimeondoka na wachezaji 22 benchi la ufundi pamoja na baadhi ya watu kutoka kwenye Menejimeti.
Hiki hapa kikosi kamili kilichosafiri:
Makipa:
Moussa Camara, Yakoub Suleiman na Alexander Erasto
Walinzi
Shomari Kapombe, Anthony Mligo,Rushine De Reuck, Karabou Chamou, Wilson Nangu na Naby Camara.
Viungo
Allasane Kante, Kibu Denis, Elie Mpanzu, Ladaki Chasambi, Mzamiru Yassin, Neo Maema, Joshua Mutale, Jean Charles Ahoua, Morice Abraham na Daudi Semfuko
Washambuliaji
Steven Mukwala, Seleman Mwalimu na Jonathan Sowah.