Uongozi wa klabu ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Crescentius Magori na na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu umekutana na benchi la ufundi na wachezaji kuwaeleza mambo mbalimbali kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/26
Miongoni mwa vitu vilivyojadiliwa ni malengo kuelekea msimu mpya wa mashindano na nini kinatakiwa kufanyika kutoka kwa benchi la ufundi na wachezaji.
Pia katika Mkutano huo Viongozi wamewakumbusha wachezaji kuhakikisha wanafuata makubaliano ya mikataba waliyosaini na klabu ili kuondoa migogoro ambayo haina lazima.
Aidha Viongozi wameweka wazi kuwa kila mchezaji anatakiwa kuhakikisha anapigania nembo ya klabu kila atakapopata nafasi ya kucheza kwakuwa tunahitaji kufikia malengo.
Wakati huo huo malengo yetu kama klabu yanabaki yale yake kama ilivyokuwa msimu uliopita kupambania kupata mataji yote ya ndani na kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.