Tamasha letu la Simba Day mwaka huu litafanyika Jumatano ya Septemba 10 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Simba Day hufanyika Agosti 8 ya kila mwaka lakini safari hii litafanyika Septemba 10 kutokana na ufinyu wa ratiba unaotokana na michuano ya CHAN inayoendelea katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.
Tamasha la Simba Day hutumika kukitambulisha mbele ya mashabiki wetu kikosi ambacho tutakitumia katika msimu wa mashindano 2025/2026.
Kama ilivyo kawaida Tamasha la Simba Day litapambwa na burudani mbalimbali na litahitimishwa kwa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa baina yetu na timu ambayo tutaialika.
Simba Day ndio Tamasha kongwe la Klabu za mpira katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambapo mwaka huu linafikisha miaka 16 tangu lilivyoanzishwa mwaka 2009.