Kocha Mkuu Fadlu Davids amesema wapinzani wetu Gaborone United kutoka Botswana tuliopangwa nao katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika sio timu ndogo na tunapaswa kujiandaa kuwakabili.
Fadlu amesema hatujawahi kukutana nao kabla lakini tulikutana na Township Rollers na Jwaneng Galaxy ambao wanacheza nao ligi moja hivyo tutawatumia kuwafahamu vizuri.
Tazama mahojiano haya hadi mwisho Kocha Fadlu ameweka wazi furaha yake ya kucheza mechi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.