Droo ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika imekamilika na tumepangwa na Gaborone United kutoka Botswana.
Mchezo wa mkondo kwanza utapigwa Septemba 19-21 ambapo tutaanzia ugenini kabla ya kurejeana nyumbani kati ya Septemba 26-28.
Gaborone ambayo inadhaminiwa na Benki ya Botswana ndio Mabingwa wa nchi hiyo ambapo msimu uliopita walikusanya alama 66.