Bocco, Morrison, Lwanga wachuana mchezaji Bora Mei

Nyota watatu wakiwamo Nahodha John Bocco, Bernard Morrison na Taddeo Lwanga wameingia fainali ya kumtafuta mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Mei (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Kabla ya kuingia fainali wachezaji walioingia tano bora ni pamoja na Pascal Wawa na Mohamed Hussein lakini Kamati Maalumu imewachuja na kubaki na nyota hao watatu.

Bocco, Morrison na Lwanga watapigiwa kura na washabiki wetu kupitia tovuti hii rasmi ya klabu na atakayepata kura nyingi atatangazwa mshindi.

Tuzo hii inadhaminiwa na Kampuni ya Emirate Aluminium Profile na ilianza kutolewa Februari mwaka huu ambapo hutoa kitita cha Sh 1,000,000 kwa mshindi.

This poll has ended (since 3 years).
SHARE :
Facebook
Twitter

187 Responses

  1. Mchezaji bora wa mwezi may want washabiki ni:
    BERNARD MORISONI (BM) WAKILI MSOMI MZEE WA KUCHETUA CHETU CHETU.hayo ndo yangu.

  2. Naipongeza timu yangu ya Simba kwa ushindi wa jana dhidi ya Namungo Fc, na matarajio yangu ni kuchukua ubingwa na kwenda kupambana tena kimataifa.pia niitakie maandalizi mema katika michezo ijayo.
    Pia ningependa kutoa salamu zangu za pole kwa mchezaji wetu, Clotus Chota Chama kwa kufiwa na mkewe.

  3. Hongereni kwa kutushirikish kuchagua mchezaji bora wa mwezi,lkn naomba katika kumpigia kura mchezaji wetu ni bora kuwekwe stastics zake jwa msimu husika maana sio wote wanafuatilia na kutunza kumvukumbu vzr.

  4. Kiukweli nimemchagua Bocco kwakua kiwango chake kimekua sana kwa hizi siku chache japokua hawa wengine nasifu viwango vyao walistahili sana ila Bocco amekua Moto Sanaa. Naomba nishauri kidogo hapa kuhusu match ya jana, kipindi cha Kwanza tulionekana Kama tumekosa kiungo mchezeshaji ila baada ya kuingia HD mliona team ilivyoshambulia na tukapata magoli me nashauri aanze kupangwa kipindi hiki ambapo kiungo wetu mchezeshaji amepata matatizo.
    SIMBANGUVU MOJA

  5. Mimi naomba tufanye usajiri mzuri ili kuboresha kikosi chetu kwa ajiri ya msimu ujao katika mashindano yote hususani klabu bingwa

  6. Simba hii ni club ambayo inatoa hamasa kubwa kwa mashabiki kuwa na moyo wa kuweza kuendelea kutoa support kubwa na pia kuendelea kupenda mpira wa miguu.

  7. Tupo pamoja katika vipindi vyote , asante kwa kutambua mchango wa mashabiki , Simba Nguvu moja

  8. Ni Jambo jema Sana kutushirikisha ktk hili

    Ushauri wangu tunapaswa tuangalie mchezaji anapataje nafasi kupangwa na kocua na anapopangwa anakwenda kufanya Nini! Morrison amekuwa akipata nafasi za kupangwa kikosini kwa tabu Sana Lin akiingia anafanya vitu vzuri sana

  9. Big up Emirates sponsers for this awards as it motivate our players to improve their performance…but I suggest to attach the video clips that show the individual players who are in the battle performance..๐Ÿ™๐Ÿ™

  10. Tadeo Lwanga namuelewa ,licha ya kuwa viungo wanafanya kazi nzuri isiyoonekana .Natamani apewe heshima kwa kumpatia tuzo hii

  11. BM3 BM3 BM3 BM3 KWANN AIKOSE KURA YANGU KWA GAME ALOLICHEZA MWEZI HUU….BM3 BEEENAARND MOMOMOMOOORISOOOOOON

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER