Karibu Simba Anthony Mligo

Tumeendelea kuimarisha kikosi chetu kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/2026 ambapo sasa tumefanikiwa kuinasa saini ya mlinzi wa kushoto, Anthony Mligo.

Mligo tumemsajili kutoka Namungo FC kwa mkataba wa miaka mitatu huku tukiwa na matumaini nae makubwa kutokana na ubora alionao.

Mligo ni mchezaji ambaye anaijua vizuri ligi yetu kwakuwa kabla ya kujiunga na Namungo alikuwa akikitumikia kikosi cha Geita Gold.

Akiwa na Namungo msimu uliopita, Mligo alikuwa muhimili wa timu ambapo pamoja na jukumu lake mama la ulinzi lakini aliisadia timu hiyo kupatikana kwa mabao mawili (asisti).

Mligo ataondoka kesho alfajiri kuelekea nchini Misri tayari kujiunga na wenzake wanaoendelea na kambi ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa mashindano.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER