Kocha Didier Gomes amewaanzisha washambuliaji wawili Medie Kagere na Chris Mugalu katika mchezo dhidi ya Namungo utakaopigwa Uwanja wa Majaliwa leo saa 10 jioni.
Mara nyingi Kocha Gomes amekuwa akiamini matumizi ya mshambuliaji mmoja na kutumia viungo watatu wa ushambuliaji lakini kutokana na umuhimu wa mechi ameamua kuanza na Kagere na Mugalu.
Katika kiungo wa ulinzi amewaanzisha Taddeo Lwanga na Mzamiru Yassin huku viungo washambuliaji wakiwa Rally Bwalya na Luis Miquissone.
Mlinzi wa kati Kennedy Juma ameanza pamoja na Pascal Wawa akichukua nafasi ya Joash Onyango ambaye amebaki jijini Dar es Salaam akiendelea kuimarika afya yake.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12) Mohamed Hussein© (15), Kennedy Juma (26), Pascal Wawa (6), Taddeo Lwanga (4) Rally Bwalya (8), Mzamiru Yassin (19), Medie Kagere (14), Chris Mugalu (7), Luis Miquissone (11)
Wachezaji wa Akiba : Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Said Ndemla (13) Miraji Athumani (21), John Bocco (22), Hassan Dilunga (21), Bernard Morrison (3).