Rushine De Reuck ni Mnyama

Mlinzi wa kati, Rushine De Reuck amejiunga na kikosi chetu kutoka Mamelodi Sundowns kwa mkataba wa mwaka mmoja huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

De Reuck (29) raia wa Afrika Kusini ni mlinzi mwenye uzoefu mkubwa wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na hiyo ni moja ya vitu vilivyotushawishi kuisaka saini yake.

Msimu uliopita De Reuck alikuwa anachezea timu ya Maccabi Petah Tikva ya Israel na alikuwa moja ya wachezaji muhimu ndani ya kikosi hicho.

Huu ni usajili wetu wa kwanza kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/2026 na tayari amewasili nchini kuanza maandalizi (Pre Season).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER