Nahodha John Bocco amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa Robo Fainali ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa leo saa moja jioni.
Kama kawaida Kocha Didier Gomes ameendelea kuamini kwenye matumizi ya mshambuliaji mmoja na leo Bocco amepewa nafasi ya kuanza.
Kocha Gomes amepanga kutumia viungo wanne wa kushambulia ambao ni Bernard Morrison, Clatous Chama, Luis Miquissone na Rally Bwalya huku kwenye kiungo wa ulinzi akicheza Taddeo Lwanga.
Kikosi kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), David Kameta (27), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Pascal Wawa (6), Taddeo Lwanga (4), Bernard Morrison (3), Clatous Chama (17), John Bocco © (22), Rally Bwalya (8) na Luis Miquissone (11)
Wachezaji wa Akiba, Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Mzamiru Yassin (19), Said Ndemla (13), Medie Kagere (14), Chris Mugalu (7), Perfect Chikwende (23).