Mlinda mlango, Aishi Manula hatakuwa sehemu ya kikosi chetu kuelekea msimu wa Ligi 2025/2026 baada ya kumaliza mkataba wake.
Manula alijiunga nasi mwaka 2017 akitokea Azam FC na leo amehitimisha miaka nane ya kudumu kwenye kikosi chetu.
Manula ameacha alama ndani ya klabu yetu ambapo alikuwa langoni kwenye kikosi kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa miaka minne mfululizo kuanza msimu wa 2018/2021.
Katika kipindi chote cha miaka nane alichodumu nasi Manula amekuwa mchezaji mtiifu na mchapakazi kitu kilichomfanya kupendwa na mashabiki pamoja na Uongozi.
Ubora na umahili aliokuwa nao Manula umemfanya kuwa mlinda mlango namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwa kipindi chote alichokuwa nasi.
Uongozi wa klabu unamtakia Aishi kheri na mafanikio mema katika maisha yake mapya ya soka nje ya Simba.