Ni rasmi kiungo mkabaji, Fabrice Ngoma hatakuwa sehemu ya kikosi chetu kuelekea msimu ujao wa mashindano 2025/2026.
Ngoma raia wa DR Congo alijiunga na kikosi chetu kutoka Al Hilal ya Sudan Julai mwaka 2023 kwa mkataba wa miaka miwili.
Katika kipindi cha miaka miwili Ngoma amekuwa muhimili katika eneo la kiungo wa ulinzi wa timu akishirikiana vizuri na Yusuph Kagoma.
Ngoma ni mchezaji mwenye nidhamu ya hali ya juu ambapo msimu uliopita kocha mkuu Fadlu Davids alimteuwa kuwa nahodha msaidizi wa kikosi.
Uongozi wa klabu unamtakia Kheri na mafanikio mema Ngoma katika maisha yake mapya ya soka nje ya Simba